Timu ya Chelsea imepata ushindi wa kwanza wa kimashindano msimu huu chini ya kocha wao mpya Frank Lampard, baada ya kuifunga timu ya Norwich mabao matatu kwa mawili katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Lampard aliyeiongoza Chelsea kwenye michezo minne ya kiushindani, kabla ya ushindi dhidi ya Norwich ameambulia sare moja na kupoteza michezo miwili kwenye mashindano yote.
Kinda Mason Mount na Tammy Abraham ndiyo waliopeleka furaha mitaa ya Stamford Bridge kwa kupachika mabao yaliyoipa ushindi timu yao huku Norwich ikijipatia mabao yake kupitia kwa Teemu Pukki na Todd Cantwell.