Serikali ya Cape Verde imekuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kuupa uwanja wake wa Taifa jina la gwiji wa soka ulimwenguni, Pele, kama ambavyo Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino alishauri nchi wanachama kufanya hivyo.
Akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga Pele Jumatatu wiki hii, Infantino alitoa rai kwa nchi wanachama wa FIFA kuupa jina la Pele moja kati ya viwanja vilivyopo katika nchi hizo kama njia ya kumuenzi.
Taarifa ya serikali ya Cape Verde imesema imeamua kuupa jina la Pele uwanja wa Taifa wa nchini hiyo uliofahamika awali kama Estádio da Várzea.