CAF yafanya mabadiliko ya terehe ya fainali ya AFCON 2021

0
1360

Uamuzi uliofikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Confederation of African Football) ni kuwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) limerudishwa kwenye muda wake wa awali ambapo sasa toleo lijalo la fainali hizo mwaka 2021 litafanyika mwezi Januari na Februari.

Kamati ya maandalizi ya fainali hiyo pamoja na Shiirikisho la Soka Cameroon (FECAFoot)zitakapofanyika fainali hizo zimesema kuwa mashindano hayo yataanza Januari 9 hadi Februari 6 mwaka 2021.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) nchi mwenyeji iliomba fainali hizo zifanyike kipindi hicho tofauti na kile kilichokuwa kimependekezwa awali kutokana na uhalisia kwamba hali ya hewa ingekuwa mbaya kwa wachezaji katika kipindi Juni – Julai.

Mwaka 2018 fainali hizo ambazo kwa mara ya kwanza zilizoshirikisha timu 24 zilifanyika Juni-Julai ili kuepusha kugongana na ligi kuu za Ulaya.

Katika fainali hizo ambazo Algeria ilitwaa kombe ilichezwa katika kipindi cha joto kali, na kipindi kama hicho nchini kitakuwa cha mvua kali nchini Cameroon, ambapo maamuzi ya kubadili tarehe yamefikiwa baada ya majadiliano na watalaamu wa hali ya hewa, wawakilishi wa wachezaji na wakufunzi.