Mdau wa Soka na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF) Abdalah Bulembo amesema kuwa, endapo kanuni na sheria mbalimbali za kuwania uongozi ndani ya shirikisho hilo zitafanyiwa marekebisho, kutakuwa na maendeleo makubwa ya soka hapa nchini.
Bulembo ameyasema hayo mkoani Dar es salaam na kuishauri TFF kuwapa uzito sawa Wadau wote wa soka nchini wenye nia ya kuwania nafasi ya Urais ndani ya shirikisho hilo na kuhakikisha hakuna kanuni na sheria zinazowagandamiza.
Hii ni mara ya pili kwa mdau huyo wa soka nchini kuanzisha mchakato juu ya kanuni na sheria za nafasi ya Urais wa TFF, kuelekea uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika Agosti 7 mwaka huu jijini Tanga.