Bosi wa soka China jela maisha kwa rushwa

0
464

Aliyekuwa Rais wa Chama cha Soka China (CFA), Chen Xuyuan amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kupokea rushwa.

Januari 2024, Chen alikiri kuchukua rushwa yenye thamani ya shilingi (za Tanzania) bilioni 28.7, jambo ambalo mahakama imesema limetia doa kubwa kwenye soka nchini humo.

Mwendesha mashtaka aliiambia mahakama kuwa Chen alipokea fedha na vito vya thamani kutoka kwa watu ambao aliwasaidia kupata kandarasi na kuandaa matukio ya kimichezo.

Aidha, taarifa ya shirika la utangazaji la China imeeleza kuwa maofisa waandamizi wa soka watatu pia wamehukumiwa vifungo vya kati ya miaka nane na 14 kwa makosa ya rushwa.