BONDIA WA KIMATAIFA AFARIKI DUNIA

0
309

Bondia Raia kutoka Urusi Mwenye Miaka 28 , Maxim Dadashev,  amefariki dunia baada ya pambano lake dhidi ya mpinzani wake, Subriel Matias,Subriel Matias Ambaye Alimpiga Sana Kichwani Dadashev mpaka Kusababishiwa majeraha makubwa kwenye Ubongo

Dadashev alishindwa kuendelea na pambano hilo ambalo mkufunzi wake, Buddy McGirt, alilazimisha lisimamishwe katika raundi ya 11 baada ya bondia huyo kupokea kichapo kikali.

Pambano hilo lilipigwa Julai 20, 2019, ambapo baada ya pambano Dadashev alikimbizwa hospitali na madaktari walimfanyia vipimo na kugundua kuwa damu ilikuwa ikimvuja kwenye ubongo na kufanyiwa operesheni ya saa mbili, ambapo jana Jumanne alipoteza maisha.