Azarenka atupwa nje Australian open

0
248

Bingwa wa Wimbledon kwa wanawake Elena Rybakina ametinga fainali ya michuano ya wazi ya Tenisi ya Australia baada ya kumbwaga bingwa mara mbili wa michuano hiyo Victoria Azarenka katika mchezo wa nusu fainali.

Rybakina, 23, amepata ushindi wa 7-6 (7-4) 6-3 na kumaliza matumaini ya Azarenka kushinda taji hilo kwa mara nyingine baada ya miaka 10 kupita.

Rybakina atacheza fainali na mshindi wa pambano lingine la nusu fainali baina ya Aryna Sabalenka ama Pole Magda Linette siku ya Jumamosi.