Azan yaangukia pua mbele ya TBC

0
215

Timu ya soka ya Azan FC imeambulia kichapo cha mabao 4 kwa 3 dhidi ya timu ya soka ya TBC, TBC Warriors, katika mchezo wa kirafiki uliowakutanisha wanamichezo hao katika Uwanja wa Jakaya Kikwete Park uliopo Ilala jijini Dar es Salaam

Katika mchezo huo uliopigwa majira ya jioni hadi saa 1 jioni, Azan walianza kupachika bao dakika za awali za mchezo, na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, timu zilitoshana nguvu kwa kutoka sare ya bao moja kwa moja

Hadi dakika tisini za mchezo zinamalizika, TBC Warriors wameibuka na ushindi wa mabao 4 kwa 3 huku bao la nne likipatikana kwa njia ya penati, na mkwaju huo kuwekwa kimiani na mshambuliaji hatari Revocatus dakika za lala salama za mchezo

Wachezaji na viongozi kutoka pande zote mbili wamekubaliana kupata mchezo wa marudiano baada ya mchezo huo kuwa na ushindani wa hali ya juu.