Azam yaanza Mapinduzi Cup kwa ushindi

0
274

Azam FC imeiadhibu Meli 4 City goli 1-0 katika mchezo wa kundi A wa michuano ya Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.

Goli pekee katika mchezo huo limefungwa dakika ya 13 na Shabaan Chilunda.

Meli 4 City imepoteza mchezo wake wa pili baada ya kufungwa magoli 2-1 na Namungo FC katika mchezo Januari 2 mwaka huu.

Mchezo ujao wa kundi hilo, Azam FC itawakabili wakulima wa Korosho, Namungo FC ambayo tayari imefuzu Nusu Fainali ya Mapinduzi Cup, huku Meli 4 City ikipewa nafasi ya mwisho kujiuliza mbele ya Yosso Boys.