Atsu aokolewa kwenye kifusi cha tetemeko la ardhi

0
597

Mwanasoka Christian Atsu ameokolewa kutoka kwenye vifusi akiwa na majeraha kufuatia tetemeko la ardhi lililoikumba Uturuki, klabu yake ya Hatayspor imeeleza.

Atsu ambaye amewahi kuichezea Chelsea, Bournemouth na Newcastle United za nchini England alifukiwa kwenye kifusi kufuatia tetemeko hilo ambalo limeua takribani watu 5,000.

Raia huyo wa Ghana mwenye miaka 31 alijiunga na klabu hiyo Septemba 2022 akitokea nchini Saudi Arabia. Muda mchache kabla ya tetemeko hilo aliichezea klabu yake akiifungia goli la ushindi dakika ya 90.