Aliyewahi kuwa kocha wa Simba afariki dunia

0
770

Aliyewahi kuwa kocha wa viungo wa Simba SC, Adel Zrane amefariki duniani.

Zrane hadi umauti unamkuta alikuwa kocha wa viungo wa APR FC nchini Rwanda.

Taarifa ya APR FC imeeleza kuwa chanzo cha kifo chake bado haijafahamika.

Akiwa na Simba amefanya kazi na makocha tofauti akianza na Patrick Aussems, Sven Vandebroeck na Didier Gomes ambapo alikuwa kipenzi cha mashabiki kwa namna alivyoifanya timu hiyo kuwa kwenye fiziki nzuri.

Adel aliondoka Simba mwaka 2021.