Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Yanga ahamia Azam FC

0
609

Klabu ya soka ya Azam imemtambulisha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Dkt. Jonas Tiboroha kuwa Mkurugenzi wa Mpira (Football Director) ambaye atashughulika na masuala yote ya mpira wa miguu katika klabu hiyo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin “Popat” amemtambulisha Tiboroha na kusema kuwa kwa sasa klabu hiyo inaendelea kuimarisha safu ya uongozi ili kujenga taasisi imara ya kuendeleza mpira wa miguu.

Popat amesema ujio ya Dkt. Tiboroha ndani klabu hiyo utaongeza kasi ya uendeshaji wa shughuli za soka ndani ya Azam FC kutokana na uzoefu alionao katika kusimamia shughuli za mpira wa miguu.

Akizungumzia majukumu yake mapya ndani ya Azam FC, Dkt. Tiboroha amesema amejiunga katika klabu yenye kiu ya mafanikio katika soka na hivyo atashirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha timu hiyo inapata mafanikio.

Kabla ya kujiunga na Azam FC Dkt. Tiboroha amewahi kuviongoza vilabu vya Yanga, Standa United, Mbao na Mtibwa Sugar.