Ukurasa rasmi wa klabu ya Yanga umechapisha picha zinazomuonesha afisa habari wa klabu hiyo Ali Kamwe pamoja na viongozi na baadhi ya wachezaji wa Yanga wakiwa hospitalini.
Kupitia ukurasa huo klabu ya Yanga imeeleza kuwa Kwamwe alipata changamoto Jumamosi Februari 24, 2024 dakika chache kabla ya kumalizika kwa mchezo wa Yanga dhidi ya CR Belouzdad ya Algeria wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Hali hiyo illmlazimu kukimbizwa katika hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambapo kwa sasa anaendelea vizuri na yuko salama.