Album ya Harmonize yenye nyimbo 18

0
338

Mwanamuziki Harmonize kutoka Tanzania ametangaza rasmi orodha ya nyimbo 18 zitakazokuwepo kwenye Album yake mpya ya #AfroEast ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni.

Katika album hiyo inayosubiriwa kwa hamu, nyota huyo wa kizazi kipya amewashirikisha wasanii mbalimbali wakubwa kutoka ndani na nje ya Afrika kama Burna Boy, Yemi Alade, Falz, Morgan Heritage.

Wimbo wa Uno ambao unaendelea kufanya vizuri ndani na nje ya Tanzania utakuwa ni sehemu ya nyimbo 18 za album hiyo.