Klabu ya Al-Hilal ya nchini Saudi Arabia imetuma ofa ya kumsajili Lionel Messi ambayo inaelezwa kuwa kitita cha TZS Bilioni 942 kimetangwa kunasa saini ya raia huyo wa Argentina.
Wakati huo huo Messi mwenye umri wa miaka 35 anahusishwa kurudi kwenye klabu yake ya utotoni ya Barcelona huku pia ikiripotiwa kuwa Inter Miami ya Marekani inawinda saini yake.
Nahodha huyo wa Argentina amesimamishwa na klabu yake ya PSG kwa kwenda Saudi Arabia bila ruhusa, huku ikilezwa kwa miamba hiyo ya Ufaransa haina nia ya kuongeza mkataba wa Messi kwa msimu wa tatu pindi utakapomalizika majira ya kiangazi mwaka huu.
Chanzo cha habari karibu na Messi kimesema kuwa adhabu hiyo imetolewa baada ya Messi kuweka wazi kwamba anataka kuondoka, akidai kuwa klabu hiyo haina mikakati.
Aidha, chanzo hicho kimesema PSG haina ratiba ya mazoezi siku ya Jumatatu, na kwamba uamuzi wa kufanya mazoezi ulitolewa Messi akiwa tayari yupo Saudia.