TEKNOLOJIA: UINGEREZA YAGUNDUA APP YENYE KUTOA TAARIFA KUHUSU MARADHI YA FIGO.

0
494

Wanasayansi nchini UINGEREZA  wamegundua teknolojia inayoweza  kutoa taarifa kwa daktari ndani ya muda mfupi kwa mtu mwenye maambukizi ya maradhi ya figo, kupitia App ya simu ya kiganjani  inayojulikana kwa jina la DEEP MIND ili kusaidia kuongeza kasi ya matibabu kwa wagonjwa hao.

App hiyo inayotoa taarifa ndani ya dakika KUMI na NNE baada ya damu ya mgonjwa kupimwa imegunduliwa na ALPHABET raia wa UINGEREZA baada ya tafiti zilizofanywa na wataalamu wa afya kubaini ongezeko la vifo taktribani laki moja kila mwaka kutokana na maradhi hayo.

Hata hivyo inaelezwa kuwa Maradhi ya figo yanaweza kusababisha athari katika viungo vingine vya mwili iwapo  hatua za haraka hazitachukuliwa kwa mgonjwa mwenye tatizo hilo. 

Aidha imeelezwa kuwa app hiyo imefanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza katika hospitali ya ROYOL FREE iliyoko nchini humo ambapo imeonesha kuwavutia wataalamu wa afya katika kuwagundua watu wenye maambukizi kwa haraka.

Source: BBC/Emmanuel Samwel- TBC