Mpishi na mfanyabiashara wa migahawa kutoka Uganda, @mama_ds_keychen anaendelea na jaribio lake la kuvunja rekodi ya dunia ya ‘Guinness’ kwa mtu mmoja kupika muda mrefu zaidi ambapo mpaka sasa amepika kwa saa 65 na dakika 40.
Ili kuvunja rekodi ya dunia ya Guinness, Mama DS atatakiwa kupika kwa muda wa siku tano mfululizo, usiku na mchana, ili apate saa 121 za kupika.
Anayeshikilia rekodi hiyo kwa sasa ni mpishi maarufu Alan Fisher ambaye amepika kwa saa 119 na dakika 57.
Mpaka sasa Mama DS amepika vyakula aina 77.