Zoezi la sensa Mtwara laongezewa nguvu

0
161

Katika kuhakisha zoezi la sensa ya watu na makazi linafanikiwa, Ofisi ya Taifa ya Takwimu mkoa wa Mtwara imewapa kazi ya ukarani wa sensa wasimamizi wa maudhui ya sensa, ili wananchi wengi zaidi waweze kuhesabiwa ndani ya muda uliopangwa.
 
Mratibu Msaidizi wa sensa ya watu na makazi  mkoani Mtwara, Patrick Kyaruzi amesema hayo  wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la sensa linaloendelea.
 
Amesema uamuzi wa kuwapa kazi ya ukarani wa sensa wasimamizi wa maudhui ya sensa umefanyika baada ya baadhi ya wananchi kulalamika kutofikiwa kwa haraka na makarani hao wa sensa.