Zoezi la kuopoa kutoka ndani ya maji ndege ya Shirika la Ndege la Precision iliyopata ajali katika ziwa Victoria inaendelea kwa kushirikisha vikosi mbalimbali.
Ndege hiyo ilipata ajali hiyo tarehe 6 mwezi huu ikiwa katika safari zake za kawaida kutoka Dar es Salaam kwenda Bukoba, Kagera na kusababisha vifo 19 na majeruhi 24.