Zoezi la Anwani za makazi lafikia asilimia 67

0
217

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema zoezi la kuweka postikodi na anwani za makazi katika maeneo mbalimbali nchini limefikia asilimia 67.

Akizungum’za kwenye mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachotangazwa na TBC , Waziri Nape amesema hadi kufikia Mei 22 mwaka huu zoezi hilo litakua limekamilika.

Ili kufanikisha zoezi hilo, Waziri Nape amesema mkakati uliopo ni kuwatumia Wasanii mbalimbali kutoa hamasa kwa Wanannchi ili waweze kutoa ushirikiano wa kutosha kurahisisha zoezi hilo muhimu.

Ametoa wito kwa Watanzania wote kushiriki katika zoezi hilo na kwa vyombo vya habari amevitaka kutoa elimu zaidi kwa Wananchi ili wafahamu umuhimu wa zoezi hilo la kuweka postikodi na anwani za makazi.

Waziri Nape pia amewataka Wananchi kushiriki katika vikao kwenye maeneo yao ili kujadili majina ya mitaa, jambo linakaloepusha malalamiko kuhusu majina ya mitaa hiyo.