Zitto Kabwe apata ajali mkoani Kigoma

0
234

Chama cha ACT-Wazalendi kimeeleza kuwa kiongozi wa chama hicho, Zitto Zuberi Kabwe amepata ajali ya gari akiwa njiani akitokea Kata ya Kalya kuelekea Lukoma kwenye kampeni katika Jimbo la Kigoma Kusini leo Jumanne Oktoba 6, 2020.

Afisa Habari ACT-Wazalendo, Arodia Peter amesema Zitto alikuwa na watu watano kwenye gari yake na wote wako salama ingawa wamepata majeraha na wanahisi maumivu makali.

Ameongeza kuwa wote wamepata huduma ya kwanza kwenye eneo la ajali baadaye wamepelekwa Kituo cha Afya cha Kalya kilichopo Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.