Wanafunzi wa shule ya msingi Bunge iliyopo Ilala Mkoa wa Dar es Salaam wamekabidhi picha yenye mfano wa sura ya Rais Samia Suluhu Hassan akiwa amembeba mtoto kama zawadi kwa Rais.
Picha hiyo imepokelewa na Waziri waMaendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Wanafunzi hao wa shule ya msingi Bunge wamekabidhi picha hiyo mkoani Dar es Salaam wakati wa kongamano la Makuzi na Malezi ya Awali ya Mtoto Ukanda wa Afrika Mashariki linaloendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).