Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limeandaa kipindi cha Jambo Tanzania kwa siku ya leo kuwa maalum ikiwa ni zawadi kwa Rais Samia Suluhu Hassan katika kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa.
Kwa mwezi huu wa Januari, kipindi cha Jambo Tanzania kimeandaa kampeni inayohusu utunzaji wa mazingira ikiwa imepewa jina la “Mwezi wa Mama”. Kampeni hii ni kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika utunzaji wa mazingira.
Kipindi cha Jambo Tanzania leo kinakujia moja kwa moja kutoka shule ya msingi Mikocheni A iliyopo mkoani Dar es Salaam.
Kaa mkao wa kupokea yale yote tuliyokuandalia kwa siku hii ya leo katika kipindi cha Jambo Tanzania, Jambo Maalum.
Heri ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan