Zanzibar yatangaza ongezeko la visa 23 vya maambukizi ya corona

0
659

Wizara ya Afya Zanzibar imetangaza ongezeko la wagonjwa wapya 23 wenye maambukizi ya virusi vya corona, hivyo kufanya idadi ya visa vilivyoripotiwa kuwa na maambukizi hadi sasa kufikia 58, kutoka 35 waliotolewa taarifa Aprili 17 mwaka huu.

Wizara ya afya imeeleza kuwa kati ya wagonjwa hao wapya, wagonjwa 21 ni raia wa Tanzania, mmoja ni raia wa Ufaransa na mmoja ni raia wa Cuba, wote wakazi wa visiwani humo.

Aidha, agonjwa wawili kati ya wagonjwa hao wapya wamefariki wakiwa majumbani mwao kabla ya kuchukuliwa vipimo, hivyo kufanya idadi ya waliofariki kwa maambukizi ya homa ya mapafu (COVID-19) kufikia watatu.

Wakati huo huo, serikali imeendelea kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa huo, huku ikiwahimiza wenye dalili kutoa taarifa mapema na kuepuka kujichanganya na watu wengine ili kudhibiti maambukizi.