Zaidi ya watu 50,000 kupata chanjo

UVIKO - 19

0
154

Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule amewaongoza wakazi wa Mkoa wa Geita kuchoma chanjo ya UVIKO 19 ambapo kwa Mkoa huo unatarajiwa zaidi ya watu 50,000 watapata chanjo hiyo kwasasa.

Senyamule amesema hayo wakati akizindua Chanjo hiyo leo katika ukumbi wa Gedeco halmashauri ya Mji Geita na amesema Mkoa huo umetenga jumla ya vituo 18 Mkoani Geita hivyo wananchi waendelee kujitokeza kwenda kupata chanjo hiyo na ametoa onyo kwa watoa huduma za afya kutotoza fedha kwa ajili ya Chanjo hiyo.

Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Geita Flavian Kasala amesema binafsi ameunga mkono na amewaomba watanzania waendelee kuliombea taifa na ameishukuru Serikali kuleta chanjo hiyo.