Rais Samia Suluhu Hassan amesema nchi imepigwa na wimbi la tatu la Covid-19 na kwamba hadi juzi kulikuwa na wagonjwa zaidi ya 100.
Rais amesema hayo leo, Ikulu Dar es Salaam alipokuwa na mkutano na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Kati ya watu hao Rais Samia ameweka wazi kuwa 70 wanatumia mitungi ya gesi na kuwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kubwa dhidi ya ugonjwa huo.
Katika kukuza uelewa na tahadhari dhidi ya Corona, waandishi wa habari wametakwa kuwa wabunifu katika kutoa elimu.
Serikali imeeleza kuwa itaendelea kutoa taarifa za mwenendo wa ugonjwa wa Corona kwa wananchi kwa kushirikiana na vyombo vya habari.