Uongozi wa Klabu ya Yanga umeeleza kuwa umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya mabadiliko ya muda wa mchezo wao dhidi ya Simba SC yaliyotolewa na TFF, kutoka saa 11:00 jioni kwenda saa 1:00 jioni.
Katika taarifa iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano ya Yanga imefafanua kuwa mabadiliko hayo yamekiuka Kanuni ya 15 (10) za Ligi Kuu ambayo inataka kuwa mabadiliko yoyote ya muda wa mchezo yatajulishwa ipasavyo kwa pande zote mbili angalau saa 24 kabla ya muda wa awali.
Kutokana na uamuzi huo, Yanga imesema kwamba itapeleka timu uwanjani katika muda wa awali (saa 11:00 jioni).
Klabu hiyo imeitaka Bodi ya Ligi na TFF kuendesha ligi kwa kuzingatia na kuheshimu kanuni zilizowekwa.