Kufuatia uwepo wa taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayosema kuwa Bonde la Olduvai Gorge lipo nchini Kenya. Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia ukurasa wa Instagram imesisitiza kuwa Bonde hilo lipo nchini Tanzania.
“Bonde maarufu la Olduvai Gorge limeendelea kuwa gumzo duniani na pia katika Nchi za Afrika Mashariki huku baadhi ya Raia hususani kutoka Nchi ya Kenya wamekua wakidai kwamba eneo hilo lipo kwao jambo ambalo sio kweli”
“Olduvai Gorge ni eneo la kihistoria linalopatikana katika eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha nchini Tanzania, eneo hilo ni Bonde lenye utajiri mkubwa sana wa historia ya chimbuko la asili ya mwanadamu”
“Katika eneo hili ambalo linapatikana nchini Tanzania pekee, Mwanahistoria Dr. Lois Leakey na Mary Leakey mwaka 1959 waligundua fuvu la kichwa cha Binadamu wa Kale ( Zinjanthropus) ambaye anasadikiwa kuishi miaka zaidi ya Milioni mbili iliyopita” Wizara ya Maliasili na Utalii.