Wizara yapania kuboresha hali za wafanyakazi

0
197

Wizara ya Maliasili na Utalii imepania kuendeleza hali bora za wafanyakazi wakati huu ambao sekta ya Maliasili na Utalii ikiendelea kuwa na nchango mkubwa katika uchumi kutokana na kuingiza fedha za kigeni kwa asilimia 25.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki wakati akifungua kikao cha 31 cha Baraza la Wafanyakazi ambapo pia amewepongeza wafanyakazi wa wizara yake na taasisi zake kwa utendaji na kufikia malengo.

Waziri, hata hivyo amewataka wajitume zaidi hasa suala la uhifadhi na kuongeza maradufu idadi ya watalii nchini.

Awali, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbas alieleza mafanikio ya kiutendaji ikiwemo wizara hiyo kuwa ya kwanza kuhamia jengo jipya katika mji wa Serikali Dodoma, kununua magari mapya na vitendea kazi vingine.

Vilevile ameshukuru Serikali kwa kuongeza bajeti ya wizara hiyo katika mwaka ujao wa fedha.