Wizara ya Fedha yabanwa Bungeni

0
124

Spika wa Bunge Dkt. Tulia Akson ameitaka wizara ya Fedha na Mipango kujibu upya swali namba 129 lililoulizwa na Mbunge Kisesa Luhaga Mpina, ambaye aliitaka serikali kutoa maelezo ya kwanini kesi 1,097 za kodi zenye thamani ya shilingi trilioni 360 na dola za Marekani milioni 181.4 hazijaamuliwa hadi sasa.

Hatua hiyo ya Spika imekuja baada ya majibu ya Naibu waziri wa Fedha na Mipango Hamadi Hassan Chande kwenda kinyume na swali la msingi la Mbunge Mpina.

Hata waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba alipojaribu kutoa ufafanuzi, maelezo yake hayakufanana na swali la msingi la Mbunge huyo wa Kisesa.

Baada ya Spika kuwahoji viongozi hao wa wizara ya Fedha na Mipango na kukosa majibu yanayoridhisha, ndipo akaamuru swali hilo likajibiwe tena kama ambavyo limeulizwa na Mbunge Luhaga Mpina.