Jeshi la Polisi Nchini linamshikilia Peter Moris mkazi wa Mlole kata ya Mwanga Kaskazini mkoani Kigoma, kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watu saba wa familia moja yaliyotokea katika kijiji cha
Kiganza mkoani humo tarehe 3 mwezi huu.
Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Nchini Liberatus Sabas amesema jeshi hilo limejiridhisha kuwa Moris amefanya mauaji hayo ambayo chanzo chake ni wivu wa mapenzi.
Amesema Moris amefanya mauaji hayo baada ya kumtuhumu marehemu January Mussa Cheche kuwa na mahusiano ya kimepenzi na mke wake.