WHO: Omicron inasambaa kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa

0
257

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limeonya kuwa kirusi kipya cha corona aina ya Omicron kinaenea kote ulimwenguni kwa kiwango ambacho haijawahi kutokea.

Maambukizi ya kirusi kipya yamethibitishwa katika nchi 77 mpaka sasa.

Mkuu wa shirika la Afya Duniani Tedros Ghebreyesus amesema kuna uwezekano mkubwa kirusi hicho kipo kwenye nchi nyingi zaidi ulimwenguni isipokuwa bado hazijakigundua.

Dkt Tedros amesema kulikuwa na wasiwasi kwamba jitihada za kutosha hazijafanyika kushughulikia kirusi hicho

“Hata kama Omicron itasababisha ugonjwa usio mkali sana, idadi kubwa ya maambukizi inaweza tena kuelemea mifumo ya afya ambayo haijatayarishwa,” amesema Ghebreyesus.

Kirusi aina ya Omicron kiligunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini mweziNovemba, na nchi hiyo inashuhudia ongezeko la maambukizi kila siku