Wezi wa vifaa vya mzani waonywa

0
234

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Ujenzi   Elius Kwandikwa amesema kuwa,  Serikali itawachukulia hatua za kisheria watu ambao wamekua wakiiba baadhi ya vifaa vilivyopo katika mradi wa mzani wa kisasa wa kupima uzito wa magari uliopo Dakawa  mkoani Morogoro.

Naibu Waziri Kwandikwa ametoa kauli hiyo mkoani Morogoro,  baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Kaimu Meneja wa  Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)  mkoani huo Mhandisi Godwin Andalwisye, taarifa inayoeleza kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ile ya wizi wa vifaa katika mzani huo wa Dakawa.