Wenye iPhone X kuna ujumbe wenu hapa

0
464

Kampuni ya Apple inayotengeneza simu za iPhone imeongeza simu toleo la iPhone X kwenye idadi ya bidhaa ambazo zinakaribia kukosa huduma ya maboresho kutoka katika maduka yao maalumu ya matengenezo.

Hii inamaanisha kuanzia sasa utaweza kutengeneza simu yako katika maduka yao maalumu lakini kutokana na uwepo wa spea utakazozipata, na kama utazikosa basi inaweza kuwa ndio mwisho wa simu yako sababu Apple hawatengenezi tena vitu vipya kuhusu toleo hilo la iPhone X.

Baada ya miaka miwili kuanzia sasa, Apple wataacha kupokea kabisa maboresho ya simu hizo.

Vifaa vingine vilivyoongezwa ni spika janja za HomePod za mwaka 2020 pamoja na Airpods za mwaka 2016.