Waziri Ummy Mwalimu atangaza visa 14 vipya vya Corona

0
1032

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ametangaza ongezeko la waathirika wapya 14 wenye maambukizi ya virusi vya corona, hivyo kufanya idadi ya visa vilivyothibitishwa nchini kufikia 46.

Katika taarifa ya wizara, Ummy Mwalimu amesema kuwa wogonjwa wote ni raia wa Tanzania, na kati yao, wagonjwa 13 wapo jijini Dar es Salaam, huku mmoja akiwa jijini Arusha.

Waziri huyo amesema kwamba wagonjwa wote wanaendelea vizuri na ufuatiliaji wa watu waliokuwa karibu na wagonjwa hao unaendelea.

Katika hatua nyingine amewahimiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo, kama vile kuepuka mikusanyiko ya watu, kunawa mikono kila mara, kufunika mdomo na pua wanapokohoa au kupiga chafya, na kufuata maagizo ya serikali.