Waziri Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amelipongeza Shirika la Utangazaji Tanzania TBC kwa maboresho makubwa ya Studio, Vipindi na uwekezaji wa mitambo ambayo imeongeza mvuto kwa Wananchi.
Waziri Nape amesema hayo wakati akitembelea Ofisi za TBC zilizopo Mikocheni Dar es salaam na kutembelea studio za TBC1 na TBC2
Pamoja na mengine waziri Nape amejionea jengo kubwa jipya ambalo ni studio za channeli ya TBC2 ambayo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni
Aidha Waziri Nape awataka watumishi wa TBC wazidi kuwa na ushirikiano Katika utendaji kazi wakati Serikali ikiwa kwenye mchakato wa kukamilisha kuundwa kwa bodi ya wakurugenzi itakayosaidia kurahisisha mambo mengi kufanyika kwa wakati
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Dkt Ayub Rioba Chacha ameshukuru ujio wa Waziri Nape ambapo amesema TBC inaendelea kuboresha usikivu kwa baadhi ya mikoa hapa nchini ambapo utafikia asilimia 83 kwa maeneo ambayo yalikuwa na changamoto ya usikivu
“Tunashukuru Sana Rais kwa Kumteua waziri Nape Nnauye maana hii Wizara aliwahi kuitumikia na kuna mambo mazuri alikuwa ameanza kuyafanya, tunaamini sasa ni muda muafaka atayatekeleza ukizingatia naye ni mwanahabari anaijua vyema Tasnia ya Habari” ameongeza Mkurugenzi Mkuu Dkt Rioba