Waziri Nape aahidi mazuri kwa wamaliki wa mitandao ya simu nchini

0
191

Serikali Kupitia Wizara Habari Mawasiliano na teknolojia ya Habari imewahakikishia wawekezaji Katika Sekta ya hanbari kuwa itashirikiana nao katika kuweka mazingira rafiki ya kiutendaji ili kutoa huduma bora kwa watanzania

Hayo yamesemwa na waziri wa Habari, mawasiliano na teknolojia ya Habari Nape Nauye mara baada ya kufanya ziara ya kikazi kwenye makampuni ya simu Jijini Dar es salaam kwa lengo la kutaka kufanya nao Kazi kwa Karibu kama Wadau muhimu kwenye Sekta ya Habari.

Waziri Nape amesema kuwa Serikali ipo tayari kuboresha sera, sheria na kanuni ili kuangalia namna ya kusaidia ufanisi kwa watoaji na watumiaji wa huduma za mawasiliano hapa Nchini.

“Ng’ombe tunayetaka kumkamua maziwa lazima tumshibishe Ili na kesho tumkamue. Niwaombe Sana kwa Serikali ya awamu hii ya sita, naomba tuondoe kutoaminiana na tuongeze kuaminana ili tufanye Kazi kwa maslahi mapana ya Taifa” ameongeza Waziri Nape

Aidha Waziri Nape amewataka makampuni ya simu nchini kushughulikia kero za watumiaji wa mitandao yao hasa uhalisia kwenye makato ya MB Ili kupunguza malalamiko ambayo yamekuwa yakiongezeka kila Wakati.