Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida ameondolewa katika eneo la Wakayama alikokua akifanya mkutano wa hadhara, baada ya kile kinachodaiwa kuwa ni kurushiwa bomu la machozi.
Habari kutoka nchini Japan zinaeleza kuwa. Kishida ameondolewa katika eneo hilo bila kujeruhiwa.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema walimuona mtu mmoja akirusha kitu na kufuatiwa na moshi, huku mwingine akisema walisikia kishindo kikubwa.
Picha za video zilizosambaa katika vyombo mbalimbali vya habari vimewaonesha maafisa wa vikosi vya ulinzi na usalama waliokuwepo katika eneo hilo wakimkamata na kumshambulia mtu anayedaiwa kuhusika na tukio hilo.
Wakati tukio hilo linatokea, Kishida ndio alikua ameanza kuhutubia katika eneo hilo la
Wakayama ambalo ni la wavuvi