Waziri Mkuu Majaliwa Awasili Katesh

0
187

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameelekea katika Mji wa Katesh, ulioko wilayani Hanang ambapo atawajulia hali waathirika wa mafuriko yaliyoambatana na maporomoko ya udongo, kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia jana wilayani humo na kusababisha vifo vya watu 49 hadi sasa na kujeruhi wengine 85.