Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amekuwa kiongozi imara akopa kwa ajili ya maendeleo na sio kinyume na hapo.

0
157

Akitoa salamu zake wakati wa hafla ya upokeaji taarifa ya Matumizi ya Fedha za Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO -19, Waziri Mkuu amesema, kwa sasa kila mahala utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa madarasa umekwenda vizuri na kwa kiwango cha juu.

Aidha Waziri Mkuu amemuahidi Rais kuwa ataendelea kusimamia kazi iliyobaki ili iweze kukamilika na kuwahudumia wananchi kwa haraka.