Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Awataka Watanzania Kuwalinda Watalii

0
287

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Bashay, wilayani Karatu wawalinde watalii ili waitangaze vema nchi ya Tanzania pindi wanaporudi makwao pamoja na kutumia fursa zinazojitokeza kwenye sekta ya utalii kuboresha maisha yao.

Waziri mkuu ameyasema hayo baada ya kuzindua mradi wa ujenzi wa vituo vya polisi vya kupunguza changamoto kwa magari ya utalii barabarani yaani huduma za usalama kwa watalii baada ya kuwepo kwa malalamiko ya magari ya watalii kusimamishwa mara kwa mara kukaguliwa na askari wa usalama barabarani.

Vituo vingine vitatu vinavyoendelea kujengwa mkoani Arusha ni katika maeneo ya Kikatiti (Arumeru), Makuyuni (Monduli) na Engikaret (Longido).

Pia Waziri mkuu amekabidhi gari la polisi kwa ajili ya doria ya watalii katika eneo la Bashay, wilayani Karatu, mkoani Arusha.