Waziri Mkuu awasihi Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari za magonjwa

0
163

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Watanzania wana jukumu kubwa la kumuenzi Balozi John Kijazi kwa kutenda yale yote mema aliyokuwa akitenda.

Aidha, amesema jukumu jingine ni kuendelea kuiombea familia yake, hasa katika kipindi hiki kigumu.

Akitoa salamu za serikali kwenye mazishi ya Balozi John Kijazi amesewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuliombea Taifa kama ambavyo Rais Dkt. Magufuli alihimiza jana, na kwamba jana Waislamu walitimza, leo Wasabato na kesho anaamini wengine wataendelea.

Amesema serikali inawapenda wananchi wake na inaendelea kufuatilia magonjwa yote, lakini wananchi waendelee kuchukua tahadhari ikiwemo kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono na kuvaa barakoa.

Kuhusu ugonjwa wa Corona amesema inafahamika kwamba hii ni vita na imeanzia kwa wakubwa na bado inaendelea, hivyo ni vyema wananchi wakajiridhisha na vitu wanavyotumia ikiwemo barakoa, kama ambavyo Rais Magufuli amewahi kutahadharisha