Waziri Mkuu atoa Tuzo ya Kiswahili kwa Washindi

0
207

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa ametoa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati -Cornell ya Fasihi ya Afrika kwa washindi wa mwaka 2021 jijini Dar es Salaam.

Amesema dhamira ya Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya kutekeleza mkakati wa kubidhaisha lugha ya Kiswahili Kitaifa na Kimataifa, ambao utazinduliwa hivi karibuni na kuwa itafanikiwa ikiwa wadau wote watajitoa kwa dhati kutekeleza mkakati huo na kusimamia maendeleo ya lugha hii adhimu na aushi.

Aidha, Majaliwa amesema Kiswahili kimetambuliwa kimataifa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kutangaza tarehe 7 mwezi Julai, kila mwaka kuwa Siku ya Kiswahili Duniani ambapo ameitaka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuanza kuandaa wiki ya maadhimisho ya Kiswahili katika siku ya mwaka huu.

Kuhusu washindi, katika kundi la Riwaya Halfani Sudy ameibuka kuwa mshindi wa kwanza, Mohamed Omary ameibuka mshindi wa kwanza kundi la shairi, wakati Mbwana Kidato ameibuka mshindi wa pili katika kundi la tamthilia na Lukas Lubungo kuwa mshindi wa pili kwenye kundi la hadithi za kubuni.