Waziri Mkuu ataka kufunguliwa kwa Bandari ya Kagunga

0
165

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa muda wa siku 14 kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuhakikisha bandari ya kimkakati ya Kagunga iliyoko mkoani Kigoma inatoa huduma ifikapo Januari Mosi mwaka 2021.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo mkoani Kigoma alipofanya ziara bandarini hapo na kukuta haitoi huduma yoyote wakati ujenzi wake ukiwa umekamilika.

Ujenzi wa bandari hiyo umegharimu Shilingi Bilioni 13.8 na umekamilika tangu mwaka 2017 ukihusisha ujenzi wa jengo la abiria pamoja na lile la mizigo

Wakati huohuo Waziri Mkuu Majaliwa amekagua soko la kisasa la Kagunga na kuagiza lianze kazi mara moja baada ya kujiridhisha kuwa limekamilika.