Waziri Mkuu ataja hatua za kufuatwa kupambana na moto shule za Kiislamu.

0
264

Kufuatia matukio ya moto ya kufuatana yaliyotokea kwenye mabweni ya shule za kiislamu hivi karibuni, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema shule hizo zinatakiwa kuwa vifaa mbalimbali vya kudhibiti moto ikiwemo vihisi moto.

Waziri Mkuu ameyazungumza hayo katika baraza la Eid lililofanyika viwanaja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam na kuwaomba viongozi wa shule kuhakikisha shule zinakuwa na vifaa ili kuhakikisha madhara yanayosababishwa na moto yanapungua.

Aidha amesema mabaraza ya kiislamu yashirikiane na mamlaka za serikali ikiwemo wakala wa ufundi na umeme (TEMESA) katika kuhakikisha usalama unakuwepo.

Pia amewapongeza vijana wa kiislamu waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kuwahakikishia kuwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakuna ubaguzi wa rangi wala dini kila mtu ana haki sawa.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa amewashukuru viongozi wa dini kwa kushirikiana na Rais wa Tanzania kupigana na janga la corona kwa kuendesha maombi maalum ya siku tatu yaliyotangazwa kufanyika kitaifa.