KitaifaWaziri Mkuu aongoza mazishi ya mbunge Atashasta NditiyeBy TBC - February 15, 20210341ShareFacebookTwitterWhatsAppLinkedin Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Ibada ya kumwombea aliyekuwa Mbunge wa Muhambwe, Mhandisi Atashasta Nditiye kwenye Kanisa la Anglikan, Kibondo Mkoani Kigoma, Februari 15, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waombolezaji wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Ibada ya kumuombea aliyekuwa Mbunge wa Muhambwe, Mhandisi Atashasta Nditiye kwenye Kanisa la Anglikan, Kibondo, Februari 15, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mbunge wa Muhambwe, Mhandisi Atashasta Nditiye katika Ibada ya kumwombea marehemu iliyofanyika kwenye Kanisa la Anglikan Kibondo, Februari 15,2021. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Muhambwe, Mhandisi Atashasta Nditiye katika mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya familia, Kibondo mkoani Kigoma, Februari 15, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima baada kuweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Muhambwe, Mhandisi Atashasta Nditiye katika mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya familia, Kibondo mkoani Kigoma, Februari 15, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)