Waziri Mkuu amwakilisha Rais Samia Japan

0
384

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Jumamosi, Septemba 24, 2022) kwenda Tokyo, Japan ambako atamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mazishi ya ya kitaifa ya Waziri Mkuu mstaafu nchi hiyo, Shinzo Abe.

Taratibu za kutoa heshima za mwisho zinatarajiwa kufanyika Jumanne, Septemba 27, mwaka huu kwenye ukumbi wa Nippon Budokan.

Waziri Mkuu huyo mstaafu aliuawa Julai 8, mwaka huu kwa kupigwa risasi akiwa kwenye mkutano wa kampeni za kisiasa katika jiji la Nara nchini humo.

Abe ambaye anatajwa kuwa kiongozi aliyeshika wadhifa wa Waziri Mkuu wa Japan kwa muda mrefu katika historia ya Japan, aliingia madarakani kuanzia mwaka 2006 hadi 2007 na akarudi tena mwaka 2012 hadi 2020.

Akiwa Japan, Waziri Mkuu atakutana na Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida.