Waziri Mkuu amfagilia mwakilishi wa UNICEF

0
504

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amempongeza mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), – Maniza Zaman kwa kazi kubwa inayofanywa na shirika hilo hapa nchini.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa pongezi hizo jijini Dar es salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Maniza.

Amesema kuwa Maniza ameonyesha upendo wa dhati kwa  watoto wa Tanzania hasa katika kusimamia masuala ya Afya, Elimu na Haki za mtoto wa kike.

Kwa upande wake Maniza ambaye amekaa nchini kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu,  ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano iliompatia kwa kipindi chote alichokuwa hapa nchini.

Amesema kuwa  moja ya mafanikio anayojivunia ni kazi ya kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri usiozidi miaka mitano ambayo imefanyika kwa kushirikiana na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) na kufanikiwa kusajili watoto wengi na kupatiwa vyeti ndani ya siku moja,  zoezi lililoendeshwa katika mikoa 13 nchini.