Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na wakuu wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Ruvuma, pamoja na watendaji wa Bodi ya Korosho Nchini kwa lengo la kujadili bei ya korosho.
Mkutano huo ulioshirikisha wakuu hao wa mikoa ambao mikoa yao imeanza kuuza korosho, pia umehudhuriwa na Wenyeviti wa vyama vikuu vya Ushirika katika mikoa hiyo na Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumba.