WAZIRI MKUU AKAGUA MAGOGO HARAMU

0
185

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua magogo katika  kijiji cha Wachawaseme ambayo yamevunwa kinyume cha utaratibu na watu wasiojuliakana kutoka katika Pori la Akiba  la Igombe wilayani Kaliua mkoa wa Tabora.

Pia, amekagua mipaka ya pori hilo na kuwasihi wanakijiji kuulinda msitu ulio katika pori kwa kuacha kukata miti ili kulinda uoto katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuacha kuendesha shughuli za kilimo, uvuvi na makazi.